Inapakia...

ELIMISHA. IMARISHA. WEZESHA.

Mradi wa “Cocoa for Schools” umejitolea kuboresha maisha ya maelfu ya wakulima wa kakao na familia zao katika wilaya za Kyela, Busokelo na Rungwe mkoani Mbeya, nchini Tanzania. Kuwekeza katika elimu ni sehemu kubwa ya programu hii kwa sababu imeonyeshwa kuwa njia pekee iliyo na matokeo zaidi ya kuweza kujikwamua na umaskini.

Kupitia mradi wa "Cocoa for Schools", kampuni ya Kim’s Chocolates hufanya kazi kwa bidii kuboresha miundombinu ya elimu katika vijijini. Lengo letu ni kujenga, kukamilisha au kukarabati katika miaka 10-12 ijayo takriban vyumba vya madarasa 2100, ofisi za walimu na kusambaza takriban vitabu vya kiada 430,000. Zaidi ya elimu, mradi huu pia husaidia wakulima kwa njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwafundisha ujuzi wa kilimo, kusambaza miche mipya ya kakao na kuwapa vifaa vya kuzalisha umeme wa nishati ya jua.